Mfanyabiashara na kiongozi wa upinzani kutoka jimbo la zamani la muungano wa Kisovieti la Tajikistan ameuwawa kwa kupigwa risasi moja kichwani mjini Istanbul baada ya kula chakula cha usiku na rafiki yake.
Shirika la habari la Uturuki la Anadolu limesema Umarali Kuvvatov ameuwawa na rafiki yake huyo barabarani katika mtaa wa Fatih wakati wa usiku baada ya kuzozana.
Shirika hilo la habari ambalo ni la binafsi linaloendeshwa na serikali limesema mke wa Kuvvatov na watoto wake wamepelekwa hospitali na gari la kubebea wagonjwa baada ya kupata mshtuko. Kuvvatov alikuwa mtu wa karibu kwa Rais Emomali Rakhmon lakini walihasimiana na akaikimbia Tajikistan mnamo mwaka 2012. Serikali ya Tajikistan hapo mwezi wa Januari iliitaka serikali ya Uturuki imrudishe nchini humo mpinzani huyo ili akakabiliwe na mashtaka ya udanganyifu na uchochezi wa kisiasa.